IQNA

Maonyesho ya Qur'ani Iran kufanyika kwa njia ya Intaneti kuanzia Mei 1-11

15:02 - April 11, 2021
Habari ID: 3473801
TEHRAN (IQNA)-Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran mwaka huu yatafanyika kwa njia ya intaneti kuanzia Mei 1 hadi 10.

Morteza Khedmatkar, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Qur'ani katika Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran amesema wanaotaka kushiriki katika maonyesho hayo wanaaza kujisajili Jumatatu na zoezi hilo litaendelea kwa muda wa siku tano.

Amesema maonyesho hayo yamepangwa kuanza tarehe 18 hadi 27 katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani mwaka jana yalifutwa kutokana na janga la COVID-19 lakini mwaka huu maonyesho hayo yanafanyika kwa njia ya itaneti.

Khedmatkar amesema mauzo katika maonyesho hayo ya Qur'ani yatafanyika kwa njia ya itaneti ambapo mashirika yanayouza bidhaa yanalazimika kupunguza bei kwa asilimia 20.

Maoneysho hayo huandaliwa kilwa mwaka na Wizara ya Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu nchini Iran.

Kutokana na janga la corona, shughuli nyingi duniani sasa zinafanyika kwa njia ya intaneti jambo ambalo limepelekea ongezeko kubwa la mauzo ya bidhaa kwa njia hiyo.

3963636

captcha