IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran kufanyika kupitia intaneti

12:59 - May 09, 2020
Habari ID: 3472748
TEHRAN (IQNA) – Duru ya 28 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran itafanyika kwa njia ya intaneti.

Maonyesho hayo huandaliwa na Idaraa ya Qur’ani na Etrat ya Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na iliakhirishwa na kasha kubatilishwa kutokana na kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Mkuu wa Idara ya Qur’ani na Etrat Abdul Hadi Faqihzadeh amesema wameamua kuwa mwaka huu maeonyesho hayo sasa yatafanyika kwa njia ya intaneti.  Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa, mapatano sasa yatafanyika mwezi wa Juni na huo utakuwa ni uzoefu mzuri na wenye manufaa.

Ameongeza kuwa, maonyesho hayo kwa njia ya intaneti pia nayo yatakuwa ya kimataifa.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran hufanyika kila mwaka kwa lengo kustawisha ufahamu wa Qur’ani na kuimarisha harakati za Qur’ani.

3896554

captcha