IQNA

Hali nchini Yemen katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani + Picha

21:48 - April 16, 2021
Habari ID: 3473820
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Yemen wanajumuika pamoja misikitini katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na kuwa nchi yao inakabiliwa na hujuma ya kinyama ya muungano vamizi wa Saudia-Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa,  katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Wayemen wenye uwezo wanawasaidia pia watu masikini nchini humo. Hivi sasa kutokana na hujuma ya Saudia, idadi kubwa ya watu wa Yemen wanakumbwa na hali ngumu ya kiuchumi. Haj Mahir  Owaid, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametoa wito kwa wahusika wote kujitahidi kukidhi mahitaji ya wananchi katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wayemen pia wamejitokeza kwa wingi misikitini ambapo wamekithirisha ibada na qiraa ya Qur’ani Tukufu.

Mwezi Machi 2015, Saudi Arabia ikiungwa mkono na Marekani, UAE na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro nchi hiyo wa nchi kavu, baharini na angani ambao unaendelea hadi sasa.

Vita hivyo vya Saudia vimesababisha maafa makubwa zaidi ya kibinadamu nchini Yemen.

Kwa mujibu  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA),  vita vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen vimepelekea zaidi ya watu 233,000 kupoteza maisha katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Idadi kubwa ya raia hasa wanawake na watoto ni waathirika wakuu wa hujuma za Saudia dhidi ya Yemen.

Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilisema kati ya Januari na Juni 2021, asilimia 54 ya Wayemen, yaani watu milioni 16.2, watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na vita vya Saudia dhidi ya nchi hiyo.

 

3964535

captcha