IQNA

16:08 - April 11, 2021
News ID: 3473803
Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kitendo cha Saudia kuendeleza mzingiro dhidi ya Yemen katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kitendo kilicho dhidi ya ubinadmau.

Msemaji wa Harakati ya Ansarullah Mohammad Abdul Salam ametuma ujumbe wa Twitter na kusema huku Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukikaribia, uhasama wa Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen unaendelea kwa mwaka wa saba mfululizo.

Ameongeza kuwa, hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen haizingatii maadili ya ubinadamu na kwamba Wayemen kwa msaada wa Mwenyezi Mungu wataendelea kulinda haki zao za kisheria, uhuru, heshima na mamlaka ya kujitawala.

Mwezi Machi 2015, Saudi Arabia ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro nchi hiyo wa nchi kavu, baharini na angani ambao unaendelea hadi sasa.

Wizara ya Haki za Binadamu ya Yemen imetangaza kuwa raia 43,582 wameuliwa moja kwa moja na majeshi ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia tangu muungano huo ulipoanzisha hujuma za kijeshi dhidi ya nchi hiyo.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni  na wizara hiyo imeeleza kuwa, maelfu ya mashambulio ya kijeshi yaliyofanywa na muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia yamesababisha vifo vya watu 43,582 wakiwemo watoto 7,999 na wanawake 5,184. Idadi ya waliopoteza maisha kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na vita hivyo ni kubwa zaidi. Kwa mujibu  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA),  vita vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen vimepelekea zaidi ya watu 233,000 kupoteza maisha katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilisema kati ya Januari na Juni 2021, asilimia 54 ya Wayemen, yaani watu milioni 16.2, watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na vita vya Saudia dhidi ya nchi hiyo.

/3474420

Tags: yemen ، ramadhani
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: