Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bw. Morteza Pirani Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania ametangaza kuzinduliwa kanali hiyo kwa kusema: “Kanali hii ya kufunza Qur’ani Tukufu nchini Tanzania inajulikana kama “Quran in Tanzania” na imezinudliwa katika mtandao ya YouTube.” Amesema kanali hiyo ilianza shughuli zake katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo katika siku 30 za mwezi huo Mtukufu kila siku klipu za mafundisho ya Qur’ani zilikuwa zikiwekwa.
Bw. Pirani amesema kanali hiyo ya YouTube itakuwa inatoa mafunzo kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika eneo zima la Afrika Mashariki.
Kanali hiyo mpya ya Qur’ani inapatikana katika anuani ifuatayo
www.youtube.com/channel/UC۶ZpMx_i۵XXnhQpIOapTAwg