IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Qari wa Iran kushiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tanzania

15:40 - March 22, 2024
Habari ID: 3478557
IQNA – Awamu ya 20 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani nchiniTanzania yatang’oa nanga jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi.

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ndicho kitakuwa mwenyeji wa hafla hii ya kimataifa ya Qur'ani ambayo inafanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wasomaji wa Qur'ani kutoka nchi mwenyeji pamoja na Misri, Uturuki, Afrika Kusini, Morocco, Palestina, Kenya, Bangladesh, Vietnam, Greenland, Iran, Msumbiji na Visiwa vya Comoro watachuana katika mashidano hayo.

Mwakilishi wa Iran katika mashindano hayo ni Ustadh Mohsen Qassemi, ambaye amesafiri hadi Tanzania kwa uratibu na Kituo cha Utamaduni cha Iran jijini Dar es Salaam.

 Iranian Qari to Compete in Tanzania Int’l Quran Contest

Jopo la majaji linajumuisha wataalamu wa Qur'ani wanaojulikana kimataifa kama vile Sheikh Othman al-Hiwari na Sheikh Ali al-Shamisi kutoka Misri.

Mashindano hayo ni miongoni mwa matukio maarufu ya Qur'ani Afrika Mashariki, yanayoandaliwa kila mwaka na Taasisi ya Khidmatul Quran.

Ni taasisi ya Kiislamu ambayo inayofanya kazi ya kukuza utamaduni na mafundisho ya Qurani nchini Tanzania.

Mbali na kuandaa mashindano ya Qur'ani, taasisi hiyo hualika maqarii wa kimataifa  kuja Tanzania kuhudhuria programu za Qur'ani nchini humo.

Mwaka jana, qari maarufu wa Misri Mahmoud Shahat Anwar alialikwa Tanzania na taasisi hiyo kusoma Qur'ani katika vikao kadhaa.

4206599

captcha