IQNA

TEHRAN (IQNA)- Qarii Mashuhuri wa Misri Sheikh Mahmoud Shahat hivi karibuni alisoma aya za Qur’ani katika sherehe iliyofanyika kwa mnasaba wa Milad un Nabi au maadhimisha ya kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad SAW.

Sherehe hiyo ilifanyika Ijumaa iliyopita katika mji mkuu wa Misri, Cairo ambapo alisoma aya za 40-43 za Surah Al Ahzab katika Qur’ani Tukufu zisemazo”

“Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.”

“ Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru.”

“Na mtakaseni asubuhi na jioni.”

“ Yeye na Malaika wake ndio wanakurehemuni ili kukutoeni gizani mwende kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu Waumini.”

Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1984.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Kuwait, Iran, Afrika Kusini, Bahrain, Pakistan, Syria, Indonesia, Ufaransa, Uturuki,  Algeria na Ugiriki.

کد ویدیو

4007497