Katika mkesha au usiku wa kufariki Mtume Muhammad (SAW) na kuuawa shahidi Imam Hassan (AS), mpango wa "Rahmatullil Alamiyn" yaani Rehema kwa Walimwengu utaandaliwa na Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha (AS) maarufu kama Astan Quds Razavi.
Tukio hili litakuwa na usomaji wa pamoja wa Surah Muhammad.
Qiraa hiyo itafanyika Jumapili, Septemba 1, 2024, baada ya Sala ya Maghrib na Isha.
Tukio hilo litafanyika kwa wakati mmoja kwenye Haram au kaburi takatifu la Imam Ridha (AS), Imam wa Nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, maeneo mengine matakatifu, na misikiti iliyochaguliwa kote Iran.
Siku ya 28 ya Safar, ambayo ni Jumatatu, Septemba 2, ni kumbukumbu ya kufariki kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Imam Hassan (AS).
Siku ya 30 ya mwezi wa Safar, Septemba 4 mwaka huu, inaadhimishwa kama kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Ridha (AS).
4234258