IQNA

Qiraa ya Sura Al-Qadr ya qarii wa Misri Sheikh Shahat Muhammad Anwar + Video

16:08 - May 06, 2021
Habari ID: 3473883
TEHRAN (IQNA)- Surah Al-Qadr ni ya 97 katika Qur'ani Tukufu na ina aya 5.

Klipu iliyohapa chini ni ya qiraa ya Sura Al-Qadr ya qarri mashuhuri wa Misri Sheikh Muhammad Shahat Anwar ambaye alifariki dunia mwaka 2008. Aidha klipu hii ina qiraa ya wanae, Mahmoud na Anwar.

Sheikh Muhammad Shahat Anwar alizaliwa mwka 1950 katika kijiji cha Kafr el-Wazir katika jimbo la Dakahlia nchini na alianza kujifunza Qur'ani akiwa mtoto mdogo. Aliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8 na alipokuwa na umri wa miaka 10, alielekea katika kijiji cha Kafr el Maqam kujifunza Tajwidi kutoka kwa Ustadh Sayyid Ahmed Farahi.

/3474637/

Kishikizo: anwar ، qiraa ، misri ، qurani tukufu ، qadr
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :