IQNA

Mashindano ya 44 ya Kitaifa ya Qur’ani ya Iran yamalizika

22:22 - December 25, 2021
Habari ID: 3474720
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya 44 ya Kitaifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamemalizika Ijumaa mjini Tehran.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na maafisa wa harakati za Qur’ani na utamaduni akiwemo Waziri wa Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu Mohammad Mehdi Ismaili na Mkuu wa Shirika la Wakfu Hujjatul Islam Sayyed Mehdi Khamoushi.

Katika kategoria ya qiraa ya Qur’ani Tukufu upande wa wanaume washindi wa nafasi ya kwanza hadi ya tatu kwa taratibu walikuwa ni Amir Hossein Rostami wa Golestan,  Masoud Nouri na Hamid Reza Nasiri wa Tehran.

Katika kategoria ya Tartila washindi walikuwa ni , Mohammad Javad Javari wa Tehran, Mohammad Hossein Haddadzadeh wa Yazd na Mohammad Poursina kutoka Isfahan kwa taratibu.

Aidha katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu nafasi ya kwanza hadi ya tatu imechukuliwa na , Sina Tabakhi kutoka Azerbaijan Mashariki,  Hossein Khani Bidgoli na Ali Gholam Azad kutoka Zanjan.

Washindi katika kategoria ya wanawake waliohifadhi Qur’ani walikuwa ni Zahra Pourtahmasb wa Mazandaran, Fahimeh Asgharzadeh wa  Kerman na Hajar Mehralizadeh wa Isfahan.

Washindi wote katika mashindano hayo wataiwakilisha Iran katika mashindano mbali mbali ya kimataifa.

4023143

captcha