IQNA

Mashindano ya 44 ya Kitaifa ya Qur’ani ya Iran yaanza

22:06 - December 21, 2021
Habari ID: 3474704
TEHRAN (IQNA)- Fainali ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanza Jumatatu mjini Tehran.

Akihutubu katika sherehe za kufungua mashindano hayo, Mkuu wa Shirika la Wakfu la  Iran Hujjatul Islam Sayyid Mehdi Khamoushi amesema mashindano ya Qur’ani ni uwanja wa kuwafanya vijana wanufaika zaidi na mafundisho ya hiki Kitabu Kitukufu.

Katika hotuba yake, aliashiria ya aya ya 21 ya Surah al-Hashr isemayo: “Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri,”  na kusema ayah ii inatuhimizwa tuwe ni kuwenye kutafakari kuhusu Qur’ani Tukufu.

Mchujo wa Mashindano ya 44 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran ulifanyika katika miji 140 nchini na kisha katika ngazi ya mikoa ambao washindi 220 wakiwemo wanawake na wanaume wamefika katika fainali. Mashindano hayo yatamalizika Alhamisi na washindi watatunukiwa zawadi Ijumaa. Washindi katika kategoria mbali mbali wataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani katika kipindi cha mwaka moja ujao.

4022392

captcha