IQNA

Qiraa bora

Qari wa Algeria Mwenye ulemavu wa macho akisoma aya katika Sura Al-Furqan (+Video)

TEHRAN (IQNA) – Muhammad Irshad Murabaei ni qari mwenye ulemavu wa macho nchini Algeria ambaye pia ni imamu wa sala nchini humo.

Ustadh Murabaei, ambaye ana sauti nzuri, anaongoza sala katika Msikiti wa Abdul Qadir na mnamo mwaka wa 2017, aliiwakilisha Algeria katika mashindano ya pili ya kimataifa ya Qur'ani ya wenye ulemavu wa macho  nchini Iran.
Klipu ifuatayo inaonyesha usomaji wa Ustadh Murabaei wa aya ya 61 hadi 68 za Surah Al-Furqan wakati wa walipaji Tarawih katika Msikiti wa Abdul Qadir:

Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara.

Naye ndiye aliye fanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya anaye taka kukumbuka, au anaye taka kushukuru.

Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama! 

Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama. 

Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi. 

Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya. 

Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo.

Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara.