Hivi karibuni, alikuwa mgeni wa kipindi cha “Mmoja wa Watu” kinachorushwa kwenye mtandao wa Al-Hayat nchini Misri, kinachoongozwa na mtangazaji maarufu Amr al-Laithi.
Muhammad alisema kuwa amehifadhi Qur’an Tukufu kwa msaada wa Allah na pia msaada kutoka kwa wazazi wake.
Amesema anashukuru Mwenyezi Mungu kwa hali yake. Kijana huyo mwenye kipaji cha ajabu aliongeza kuwa anajitahidi kuwa mtu mwema na kuhudumia nchi yake na dini yake.
Mvulana huyo alisoma aya za Qur’an katika kipindi hicho na akaonyesha uwezo wake wa kuiga mitindo ya maqari mashuhuri.
Baadaye Muhammad pia aliimba kaswida kadhaa za kidini pamoja na wimbo wa kumsifu mama yake.
Mama yake amesema kwenye kipindi hicho kuwa kila mtu hukupata na mshangao anapoona hali ya Muhammad.
Alibainisha kuwa kuna kesi saba pekee duniani zenye aina hii ya ulemavu wa kimwili, na mmoja tu yupo Misri na Mashariki ya Kati.
“Kwa sababu ya hali ngumu na pia kwa kuwa madaktari wengi walisema Muhammad hatapona na atafariki, sikuwa na matumaini, lakini, Alhamdulillah, alinusurika na amehifadhi aya zote za Qur’an katika moyo wake .”
Aliendelea kusema kuwa sura ya mwanawe na namna watu walivyomtazama vilimfanya ahuzunike, hata hivyo, Mwenyezi Mungu alibadilisha mambo.
“Sasa watu wanampenda na wanapiga naye picha.”
Mama yake Muhammad aliwaambia akina mama wenye watoto wenye ulemavu kuwa wavumilivu, wamshukuru Mwenyezi Mungu na wasikate tamaa, kwa sababu huu ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
3492893