IQNA

Tawaf

Hija: Tawaf ya wenye ulemavu wa macho

21:53 - May 26, 2024
Habari ID: 3478886
IQNA - Katika hatua yenye mvuto na yenye kuashiria Imani thabiti, Mahujaji wawili wenye ulemavu wa macho walionekana wakifanya Tawaf kwenye ghorofa ya kwanza ya Masjid al-Haram, msikiti mtakatifu zaidi wa Uislamu iliko Ka'aba.-

Hija: Tawaf  ya wenye ulemavu wa machoWakiwa na fimbo za wenye ulemavu wa macho, walizunguka kwenye Ka’aba kwa hisia jambo ambalo linaashiria ibada hiyo ni zaidi ya kitendo cha kimwili cha kuona kwa macho. Tawaf, kitendo cha kuzunguka Al-Kaaba mara saba kwa mwelekeo kinyume na saa, ni ibada kuu ya Hija na Hija ndogo ya Umrah ni dhihirisho la kujitolea katika Uislamu. Ibada inayotekelezwa na walemavu wa macho inawakumbusha Waislamu kwamba Hija ya kweli inahusisha zaidi ya macho tu. Hisia hii ilionyeshwa waziwazi na na Mahujaji wawili, ambao uwezo wao wa kuona kimwili unaweza kuwa na kikomo, lakini mtazamo wao wa kiroho unaendana vyema na uwepo wa Mwenyezi Mungu. Ushiriki wao pia unatumika kama ushuhuda wenye nguvu wa asili ya kujumuika kwa ibada ya Kiislamu katika Masjid al-Haram.

 

Kishikizo: ulemavu wa macho
captcha