IQNA

Mashindano ya Qur'ani Iran

Zaidi ya Nchi 120 zaalikwa kuhudhuria mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

16:14 - October 24, 2022
Habari ID: 3475981
TEHRAN (IQNA) - Mialiko imetumwa kwa zaidi ya nchi 120 kwa ajili ya kushiriki katika toleo lijalo la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran, afisa mmoja alisema.

Hamid Majidimehr, ambaye ni Katibu wa Makao Makuu ya Uratibu wa Mashindano ya Qur'ani ya Iran, aliyasema hayo jana Jumapili mjini Tehran. Alisema nchi hizo zimealikwa kuwatambulisha wawakilishi wao kwa ajili ya kuhudhuria awamu ya 39 ya mashindano hayo.

Majidimehr alisema idadi kubwa zaidi ya nchi ambazo zimewahi kushiriki katika mashindnao ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran ni  84 na kuongeza kuwa, "Tunatumai rekodi hii itavunjwa na tutashuhudia uwepo wa wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 90 katika mashindano yajayo."

Alibainisha kuwa baada ya mchakato wa awali wa mchujo kukamilika, mchujo wa awali wa mashindano hayo umepangwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad mwishoni mwa Disemba.

Fainali imeandaliwa katika hafla ya Mab'ath, ambayo itaadhimishwa katikati ya Februari 2023, afisa huyo alisema. Mab'ath ni kumbukumbu ya siku ambayo Mtume Muhammad (SAW) alichaguliwa kuwa mjumbe wa Mungu.

Majidimehr aliyataja mashindano ya Iran kuwa ni mashindano makubwa zaidi na yenye sifa bora zaidi ya kimataifa ya Qur'ani duniani sio tu kwa idadi ya washindani bali pia kategoria mbali mbali za kiufundi.

Jumuiya ya Wakfu na Misaada ya Iran huandaa mashindano hayo kila mwaka kwa kushirikisha wahifadhi na wasomaji ur'ani kutoka nchi mbalimbali. Katika mashindano hayo huwa na kategoria za wanaume, wanawake, wanafunzi na wenye ulemavu wa macho.

3480968

Habari zinazohusiana
captcha