IQNA

Shakhsia Katika Qur'ani Tukufu / 28

Asiya; Mwokozi wa Musa na Mfano wa Kuigwa kwa Waumini Wanawake

18:51 - January 23, 2023
Habari ID: 3476453
TEHRAN (IQNA)- Isipokuwa Bibi Maryam, hakuna mwanamke mwingine ambaye ametajwa moja kwa moja katika Quran Tukufu. Lakini kuna majina yasiyo ya moja kwa moja ya wanawake Waumini na makafiri.

Kwa mfano mke wa Nuh (AS) na mke wa Lut (AS) wametajwa kuwa ni makafiri huku Asiya akitajwa kuwa ni mfano wa kuigwa kwa wanawake waumini, ingawa alikuwa mke wa mtawala dhalimu.

Asiya alikuwa mke wa Firauni, mfalme wa Misri ya kale, wakati Musa (AS) alipozaliwa. Baadhi ya wafasiri na wanahistoria wanasema alitoka Bani Isra’il na wengine wanasema alikuwa shangazi yake Musa (AS). Alichukua jukumu la kumwokoa Musa kutoka kwenye Mto Nile na kumwamini alipokuwa nabii.

Jina la Asiya halipo kwenye Quran lakini wafasiri wanasema maneno "Mkewe Firauni" yanayokuja mara mbili kwenye Qur'ani Tukufu yanamhusu yeye. Maneno hayo yametajwa katika aya ya 9 ya Surah Al-Qasas ambayo inahusu kumchukua Musa kutoka kwenye mto Nile na kumshawishi Firauni kumchukua. Na katika aya ya 11 ya Surah At-Tahrim, ametajwa kuwa ni mfano wa kuigwa kwa wanawake kinyume na wake wa Nuhu na Lut:

“Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalim.”

Asiya alipoona miujiza ya Musa, alimwamini. Firauni alipojua jambo hilo, alimwomba aache kumwabudu Mwenyezi Mungu lakini akakataa. Firauni aliamuru ateswe. Akawaamuru askari wake wamfunge na kupigilia misumari mikononi na miguuni mwake. Kwa mateso na masaibu haya aliaga dunia.

Katika baadhi ya Hadith, Asiya ametajwa pamoja na Hadhrat Khadija (SA) na Hazrat Zahra (SA) kuwa ni wanawake bora zaidi duniani.

captcha