IQNA

Shakhsia katika Qur’ani Tukufu /26

Harun; Mtume wa Mwenyezi Mungu na ndugu ambaye ni kigezo bora

23:14 - January 12, 2023
Habari ID: 3476394
TEHRAN (IQNA) – Utafiti wa hadithi za Mitume wa Mwenyezi Mungu unaonyesha kwamba kila mmoja wao alikuwa na sifa maalum. Harun (AS), kwa mfano, alikuwa mzungumzaji na alikuwa na uwezo wa kushawishi.

Ndiyo maana ndugu yake, Musa (AS), alimwomba Mwenyezi Mungu ampe Harun fursa ya kumsaidia katika kuendeleza Tauhidi.

Harun (AS) alikuwa nabii wa Mwenyezi Mungu na ndugu yake Musa (AS). Baba yake alikuwa Omrani na mama yake alikuwa Yokebedi. Harun alikuwa mkubwa kuliko Musa lakini aliteuliwa utume baada ya ndugu yake.

Jina la Harun limetajwa katika Sura nyingi za Quran kama vile Al-A'raf, An-Nisa, Al-An'am, Yunus, Taha, Al-Anbiya, Al-Furqan, Ash-Shua'ara, na Al-Qasas. .

Wayahudi, Wakristo na Waislamu wanaamini utume wake. Kwa mujibu wa Hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), baadhi ya dhuria wa Harun walikuwa mitume wa Mwenyezi Mungu, akiwemo Nabii Ilyas (AS).

Musa alipoteuliwa kuwa nabii na kupewa utume wa kumwalika Firauni kwenye imani ya Mungu mmoja, alimwomba Mungu amruhusu amchukue Harun pamoja naye kwa sababu alikuwa mzungumzaji na alikuwa na uwezo wa kushawishi.

Harun alikuwa na ndugu yake kila mahali na alishirikiana naye katika shughuli zote ili kumsaidia kutimiza utume wake wa kinabii. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu alimteua Harun kuwa mtume pia. Uteuzi huo pia ulikuwa baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Musa ambayo ilimsaidia katika utume wake.

Katika Hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) uhusiano wa Imam Ali (AS) na Mtume Muhammad (SAW) umefananishwa na ule wa Harun na Musa.

Harun alikuwa mahali pa Musa wakati Bani Israil walipoanza kuabudu ndama. Licha ya jitihada zake, hakuweza kuwazuia kufanya hivyo. Wote isipokuwa wachache walimpinga Harun mpaka Musa akarudi.

Kulingana na wanahistoria, Harun aliishi kati ya miaka 123 na 133 na alikufa miaka mitatu kabla ya kifo cha Musa.

Kaburi lililo juu ya mlima magharibi mwa Yordani (Jordan) linasemekana kuwa la Harun. Ndio maana Mlima Petra pia unajulikana kama Jabal Harun (Mlima wa Harun).

captcha