IQNA

Kauli mbiu ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qurani ya Iran: Qur'ani Tukufu, Kitabu cha Ustawi

15:52 - January 30, 2020
Habari ID: 3472420
TEHRAN (IQNA) – Kauli mbiu ya Maonyesho ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran itakuwa ni 'Qur'ani Tukufu Kitabu cha Ustawi."

Hayo yamesemwa na Abdul Hadi Faqihizadeh, Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani na Itrah ambaye ameongeza kuwa maonyesho hayo yamepangwa kufanyikwa kwa muda wa wiki mbili.

Aidha amesema maonyesho hayo yamepangwa kufanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu kuanza Mei 5 hadi 19 katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Irna, Tehran.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran na hufanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kustawisha ufahamu na utamaduni wa Qur'ani Tukufu nchini Iran. Katika maonyesho hayo huwa kunaonyeshwa mafanikio yaliyofikiwa na Iran na nchi zingine duniani katika sekta ya Qur'ani Tukufu.

3874369

captcha