Akizungumza Jumamosi, Abdul Hadi Feqhizadeh, Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayeshughulikia masuala ya Qur'ani amesema maonyesho hayo yatamalizika tarehe 23 au 25 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Amesema kuwa maonyesho hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA na kuongeza kuwa mwaka huu kitengo cha kimataifa cha maonyesho kitazingatiwa zaidi katika maonyesho hayo ya 28.
Maonyesho hayo ni fursa ya kutangaza mafanikio ya Iran katika uga wa Qur'ani na kubadilishana mawazo na washiriki kutoka mataifa mengine ya Kiislamu.
Mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu Iran katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.