IQNA

Taarifa ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa baada ya kuwekewa vikwazo na Marekani

21:34 - December 10, 2020
Habari ID: 3473442
TEHRAN (IQNA) - Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al MustafaSAW kimetoa taarifa na kueleza kuwa hatua ya serikali ya Markani ya kukiwekea vikwazo chuo hicho ni mfano wa wazi wa siasa za kupinga elimu.

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa kimeeleza katika taarifa kuwa hatua ya karibuni ya serikali ya Marekani ya kutangaza kukiwekea vikwazo chuo hicho cha Kimataifa cha Jamiatul Mustafa kwa mara nyingine tena kimedhihirisha sura halisi ya kupenda kujitanua na kiistikbari ya serikali hiyo. 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa kitendo cha kuiwekea vikwazo taasisi ya kielimu ambayo ni mwanachama rasmi wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Kimataifa Duniani na ambayo wanachuo wake wanatambulika duniani kama wahamasishaji wa uadilifu na kuzuia vitendo vya uchupaji mipaka; huku athari zao za kielimu zikijielekeza kwenye masuala ya amani, undugu na usawa baina ya mataifa mbalimbali hakuna maana nyingine isipokuwa ni kupinga elimu.

Taarifa ya Chuo Kikuu cha Al Mustafa imesisitiza kuwa historia inaonyesha kuwa aina hiyo ya utamaduni wa chuki haijafika popote; na wala haikuwanufaisha waasisi wake; na kwamba bila shaka, nuru ya kimaanawi, busara na kupenda uadilifu ya wanasayansi na watafiti itashinda giza la chuki, uovu, na mabavu ya ubeberu wa dunia.  

Wizara ya Fedha ya Marekani Jumanne wiki hii ilimweka katika orodha ya shakhsia na taasisi zilizowekewa vikwazo na Ofisi ya Udhibiti wa Mali za Nchi Ajinabi ya Marekani Hassan Irlu Balozi wa Iran huko Yemen na Chuo Kikuu cha Al Mustafa cha hapa nchini.

3940180

captcha