IQNA

12:25 - January 16, 2022
Habari ID: 3474812
TEHRAN (IQNA)- Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) Tawi la Tanzania kimeanza mwaka mpya wa masomo katika sherehe iliyofanyika Jumamosi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hafla hiyo imehudhuriwa na wanafunzi wa chuo hicho pamoja na wageni waalikwa wakiwemo wanazuoni wa Kiislamu nchini humo.

Kati ya walioshiriki katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam ni wanazuoni wa Kishia na Kisunni na pia wanafunzi wa vyuyo vingine vya kidini nchini humo wakiwemo wanafunzi wa  Chuo cha Dini cha Imam Sadiq (AS).

Sherehe hiyo imeanza kwa qiraa ya Qur'ani  na kisha nyimbo za mataifa ya Tanzania na Iran. Kikao hicho kimehutubiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) Tawi la Tanzania Hujjatul Islam Ali Taghavi ambaye pia alisoma ujumbe wa Rais wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) Hujjatul Islam Ali Abbasi.

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) ni chuo cha Kiislamu ambacho kilianzishwa kwa lengo la kuarifisha Uislamu kwa dunia kupitia mbinu na teknolojia za kisasa.

والمسلمین علی تقوی برای حاضران قرائت شد.

سال تحصیلی جدید نمایندگی المصطفی در تانزانیا آغاز شد + تصاویر

4028824

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: