IQNA

Hujuma 900 za chuki dhidi ya Uislamu zaripotiwa Ufaransa mwaka 2020

20:47 - February 08, 2021
Habari ID: 3473630
TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya hujuma 900 zimeripotiwa dhidi ya Waislamu na taasisi za Kiislamu kote Ujerumani katika mwaka wa 2020.

Gazeti la Neuer Osnabrücker Zeitung limeripoti kuwa jumla ya hujuma 901 zimetekelezwa Ujerumani mwaka 2020 ikiwa ni ongezeko la asilimia ikilinganishwa na mwaka 2019 wakati kuliripotiwa jinai 884 ambazo zilifungamanishwa na chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia.

Pamoja na kuwepo vizingiti katika shughuli za umma, kumshuhudiwa ongezeko la matukio ya chuki dhidi ya Uislamu kama vile kuchorwa kuhujumiwa misikiti, kuchorwa nembo za kinazi katika maeneo ya Waislamu na wanawake Waislamu kuhujumiwa na kuvuliwa hijabu na mitandio hadharani.

Mtaalamu wa masuala ya ndani katika Chama cha Kijani cha Mrengo wa Kuhoto (Die Linke) Ulla Jelpke amesema hujuma hizo ni sehemu ndogo tu ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani.

Ujerumani ni nchi yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 81 na ina Waislamu takribani milioni tano na hivyo kuifanya nchi ya pili kwa idadi ya Waislamu Ulaya Magharibi baada ya Ufaransa. Aghalabu ya Waislamu Ujerumani wana asili ya Uturuki.

Mwaka jana polisi nchini Ujerumani waliwakamata watu 12 ambao walishukiwa kuanzisha mtandano wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali kwa lengo la kutekeleza hujuma dhidi ya wanasiasa, wakimbizi na Waislamu.

Idara ya Usalama wa Taifa Ujerumani inaamini kuwa kuna karibu watu 24,100 wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia ya kufurutu ada na karibu nusu yao wako tayari kutumia mabavu na kutekeleza hujuma za kigaidi dhidi ya wakimbizi, raia wa kigeni, Waislamu na wanasiasa wasioafikiana na sera za mrengo huo wa kulia.

3473932

captcha