IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Msikiti nchini Ujerumani wapokea barua ya kutishia

11:13 - August 05, 2023
Habari ID: 3477384
BERLIN (IQNA) - Msikiti mmoja nchini Ujerumani ulipokea barua ya vitisho kutoka kwa kundi la Wanazi mamboleo siku ya Ijumaa.

Msikiti wa Eyup Sultan, ulioko Bramsche, Saxony ya Chini, ndio uliopokea barua hiyo ya kuogofya. Yaliyomo katika barua hiyo yalijumuisha ujumbe ufuatao: "Endeleeni hivi. Tuliyowatendea Wayahudi, tutawatenda ninyi pia. Siku hiyo haiko mbali."
Zaidi ya hayo, barua hiyo ilikuwa na matusi yaliyolenga Uislamu.
Ahmet Irmak, mwenyekiti wa msikiti huo unaofungamana na Muungano wa Uturuki na Kiislamu katika Masuala ya Kidini (DITIB), alifichua kuwa msikiti mwingine katika eneo hilo ulipokea barua ya vitisho kama hiyo mapema wiki hii.
Barua zote mbili zilitiwa muhuri kwa lebo "NSU 2.0," ambayo inarejelea kikundi cha Wanazi mamboleo kilichohusika na mauaji kadhaa.
Irmak alisisitiza kwamba hapo awali walikuwa wamepokea barua kama hiyo kwa njia ya barua takriban mwaka mmoja uliopita. Alielezea wasiwasi wake kuhusu vitisho hivyo na kuzitaka mamlaka kuchukua matukio haya kwa uzito.
Msikiti huo umewasilisha malalamiko  kwa polisi.
Kwa mujibu wa DTIB, mwaka jana nchini Ujerumani, takriban misikiti 35 ililengwa katika mashambulizi yaliyotekeelzwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu na pia makundi ya itikadi kali za mrengo wa kulia nchini humo.

3484634

captcha