IQNA

20:55 - November 14, 2020
News ID: 3473359
TEHRAN (IQNA)- Waendesha mashtaka nchini Ujerumani wamewafikisha kizimbani wanaume 10 wanachama wa mrengo wa kulia wa kibaguzi ambao walikuwa wanapanga kutekeleza hujuma dhidi ya Waislamu na kuipindua serikali ya Ujerumani.

Kwa mujibu wa taarifa watu hao waliofikishwa mahakamani mjini Stuttgart Ijumaa wanatuhumiwa kuunda kundi lao linalojulikana kama Group S mwezi Septemba mwaka 2019 ambapo walimiliki silaha kinyume cha sheria.

Imedokwzwa kuwa walkuwa wanapanga kuvuruga amani Ujerumani kwa kushambulia misikiti na kuua au kujeruhiwa Waislamu kwa wingi.

Aidha walipanga kuipindua serikali ya Ujerumani na kutumia mabavu dhidi ya wapinzani wao wa kisiasa.

Kesi hiyo inaendelea.

3473107

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: