IQNA

Mayahudi 300 Waethiopia wahamia aradhi zinazokaliwa kwa mabavu

21:31 - March 12, 2021
Habari ID: 3473730
TEHRAN (IQNA) - Mayahudi wengine 300 wa Ethiopia ambao ni maarufu kwa jina la Mafalasha wamehamia katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ambazo zimepewa jina bandia la Israel.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umewahamishia Mayahudi hao wa Kiethiopia na kuwaingiza katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu. Kitendo hicho za Israel ni sehemu ya njama za kiuadui za Wazayuni, za kuvuruga muundo wa kijamii wa Palestina.

Gazeti la Kizayuni la The Jerusalem Post limeripoti habari hiyo leo Ijumaa na kuongeza kuwa, Mafalasha 300 ni kundi la karibuni kabisa la Mayahudi 2000 wa Ethiopia walioingia Israel.

Mwezi Oktoba mwaka jana, Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni lilipasisha muswada wa kuhamishiwa Palestina, Mayahudi 2000 wa Ethiopia.

Utawala wa Kizayuni unatumia mbinu hiyo ya kuwahamishia Palestina Mafalasha hao kwa lengo la kuvuruga muundo wa kijamii wa Wapalestina ili ifike mahala muundo wote wa kijamii na kijiografia wa Palestina usiwe tena na sura yake ya Kiislamu na Kiarabu.

Mayahudi hao wa Ethiopia wanabaguliwa sana chini ya utawala wa Kizayuni. Kwanza hawahesabiwi kuwa daraja sawa na wakazi wengine wa utawala wa Kizayuni na pia wametengewa maeneo maalumu yenye hatari kwa ajili ya kuishi.

Eneo ambalo Mayahudi wa Ethiopia wamerundikwa zaidi ni kitongoji cha Kiryat Arba karibu na al Khalil. Vile vile karibu na Safd huko al Khalil na katika kitongoji cha Ashkelon ambapo wakazi wa maeneo hayo ni miongoni mwa wahanga wakubwa wa makombora ya Wapalestina kila utawala wa Kizayuni unapoanzisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya Wapalestina hao.

3959171

captcha