IQNA

Maulamaa Bangladesh waidhinisha kudungwa chanjo ya COVID-19 Mwezi wa Ramadhani

23:38 - March 16, 2021
Habari ID: 3473740
TEHRAN (IQNA) -Jumuiya ya Kiislamu Bangladesh imesema Waislamu wanaweza kudungwa chanjo ya COVID-19 au corona katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hakubatilishi Saumu.

Ramadhani hakubatilishi Saumu.

Jumuiya hiyo imetoa maelekezo hayo baada ya kufanya mashauriano na wanazuoni wa Kiislamu na maafisa wa afya, imesema taarifa ya Wizara ya Masuala ya Kidini ya Bangladesh siku ya Jumatatu.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Md Mushfiqur Rahman ameongeza kikao hicho cha mashauriano ambayo kimehudhuriwa na wanazuoni na wasomi wa ngazi za juu wa Kiislamu nchini humo.

Wasomi walioshiriki katika kikao hicho wameafikiana kuwa, kudungwa COVID-19 hakubatilishi Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani inadungwa katika msuli wa mkono. Wamesema aghalabu ya wanazuoni wa Kiislamu duniani wanaafikiana na fikra hiyo.

Bangladesh ilizindua kampeni ya kitaifa ya chanjo ya COVID-19 mnamo Februari ambapo tayari watu milioni 4.2 wameshadungwa chanjo hiyo kati ya watu wote milioni 163 nchini humo.

3473858

captcha