Katika taarifa Jumanne, Idara ya Fatwa za Kwa njia ya Intaneti katika Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar imesema Waislamu wanaweza kudungwa chanjo ya COVID-19 wakiwa wamefunga Saumu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Taarifa hiyo imesema chanjo zote cha COVID-19 zinalenga kuimarisha mfumo wa kinga mwilini na hazitazamwi kama chakula au kinywaji.
Pamoja na hyo Al Azhar imependekeza kuwa, ikiwezekana, wanaolenga kudungwa chanjo ya COVID-19 wafanya hivyo baada ya Futari kwa sababu yamkini baadhi ya wenye kudungwa chanjo ya Corona wakahitajia lishe ya haraka au wakalazimika kumeza dawa kutokana na athari za chanjo hiyo.