IQNA

Wanazuoni wa Kishia Afghanistan wataka utawala wa Taliban ulinde misikiti

13:19 - November 11, 2021
Habari ID: 3474542
TEHRAN (IQNA)- Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa Madhehebu ya Shia katika jimbo la Herat nchini Afghanistan wameitaka serikali ya Taliban kurejesha kamati za usalama ili kulinda misikiti ya Mashia ambayo inakabilia na tishio la kushambuliwa na magaidi wakufurushaji wa ISIS au Daesh.

Baraza hilo limetoa wito pia kwa serikali ya Taliban kuwarejeshea vijana wa kamati za kulinda misikiti. Wamesema kuwa wana wasi wasi mkubwa kuwa awana ulinzi baada ya maafisa wa utawala wa Taliban kuwapokonya vijana sialaha.

Halikadhalika baraza hilo limesema tokea utawala wa Taliban uingie madarakani mwezi Agosti, kumekuwepo na hujuma nyingi dhidi ya misikiti ambazo zimetekelezwa na ISIS.

Mwezi uliopita zaidi ya waumini sitini waliuawa shahidi baada ya kundi la kigaidi la ISIS kutekeleza hujuma dhidi ya  msikiti wa Mashia mjini Kandahar wakati wa Sala ya Ijumaa. Hujuma hiyo ilikuja wiki mbili tu baada ya magaidi hao hao wa ISIS kushambulia msikiti katika mji wa Kunduz na kuua shahidi waumini zaidi ya 100. Mamia ya watu  walijeruhiwa katika hujuma hizo mbili.

3476429/

captcha