IQNA

Ugaidi

Al-Azhar yalaani mauaji ya waumini waliokuwa msikitini Afghanistan

13:09 - September 06, 2022
Habari ID: 3475743
TEHRAN (IQNA) - Katika ujumbe wake, Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar kimelaani shambulio la kigaidi dhidi ya waumini katika msikiti mmoja ulioko katika mji wa Herat nchini Afghanistan na kulitaja kuwa ni kinyume na maadili ya kidini na kibinadamu.

Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar katika ujumbe huu, huku kikilaani mlipuko huo, kilisema: "Kuwashambulia waumini ndani ya Nyumba ya Mwenyezi Mungu ni ugaidi wa kumwaga damu na uko mbali na maadili ya kidini na ya kibinadamu."

Katika ujumbe huu, Al Azhar imesisitiza kuhusu kuratibiwa juhudi za nchi za Kiislamu na jumuiya ya kimataifa kukabiliana na ugaidi na kuutokomeza kabisa.

Katika muendelezo wa ujumbe wake Al-Azhar sambamba na kutoa salamu zake za rambirambi na masikitiko makubwa kwa wananchi wa Afghanistan na familia za wahanga, amemuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwasamehe na kuwarehemu wahanga wa tukio hilo la kuhuzunisha na kupona haraka waliojeruhiwa. Al Azhar imeelezea matumaini kwamba usalama na amani vitarejea Afghanistan na Waafghani kuwa salama kutokana na madhara ya ugaidi.

Ikumbukwe kwamba siku ya Ijumaa, mlipuko mbaya ulitokea katika Msikiti wa Ghazergah huko Herat, Afghanistan, na kusababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa.

Mlipuko huu ulitokea wakati wa mkutano wa kiuchumi uliofanyika huko Herat ambao Mullah Baradar, Naibu Waziri Mkuu wa Taliban alikuwa anahudhuria kikao hicho.

4083305

captcha