IQNA

Iran yawapokea na kuwapa matibabu majeruhi wa hujuma ya kigaidi Afghanistan

13:36 - January 23, 2022
Habari ID: 3474842
TEHRAN (IQNA)- Jumamosi usiku magaidi walishambulia mtaa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji wa Herat nchini Afghanistan ambapo watu wasiopungua saba waliuawa na wengine 10 walojeruhiwa.

Kwa mujibu wa Daktari Aref Jalali aliye mjini Herat, miongoni mwa waliouawa shahidi katika hujuma hiyo kulikuwa na wanawake wa tatu. Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na hujuma hiyo lakini magaidi wakufurishaji wa ISIS kwa kawaida huwalenga Waislamu wa madhehebu ya Shia katika eneo hilo na maeneo mengine Afghanistan.

Kufuatia ugaidi,  Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Iran mjini Herat Mohammd Siddiqi-Fur ametuma salamu zake za rambi rambi huku akisema waliojeruhiwa watapata matibabi Iran. Tayari watu watano waliojeruhiwa vibaya wameshawasili Iran kwa ajili ya matibabu.

Tokea kundi la Taliban lichukua madaraka nchini Afghanistan, kundi la ISIS limetangaza mara kadhaa kuhusika na hujuma za kigaidi.

4030585

captcha