Hayo yamesemwa na Hussein Hamhad ambaye ni miongoni mwa majaji wa kimataifa wa Lebanon na mjumbe wa kamati ya majaji wa duru ya pili ya mashindano ya kimataifa ya Qurani ya wanachuo wa Kiislamu na kuongeza kuwa kufanyika mashindano hayo nchini Iran kunaonyesha umuhimu mkubwa wa Qurani kwa viongozi, wanachuo na wananchi Waislamu wa Iran.
Hussein Hamdan ambaye alipata nafasi ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya Qurani yaliyofanyika yapata miaka 20 iliyopita nchini Iran, amesisitiza juu ya udharura wa kuimarishwa mahusiano ya Kiqurani baina ya mataifa ya Kiislamu na akasema, anatarajia kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itasaidia juhudi za kueneza utamaduni wa Qurani katika ulimwengu wa Kiislamu kwa kutoa uzoefu wake katika uwanja huo.
Msomaji huyo wa Qurani mwenye uzoefu ameashiria duru ya pili ya mashindano ya kimataifa ya Qurani ya wanachuo wa Kiislamu na akatoa pendekezo kwamba, ili kufanikisha mashindano hayo na kushirikisha zaidi nchi za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu hapana budi mashindano ya Qurani kama yale ya tarehe 27 Rajab, siku kubaathiwa kwa Mtume Muhammad SAW na yale ya siku ya kuzaliwa mwokozi wa wanadamu Imamu Mahdi AS yafanyike kwa pamoja kwa shabaha ya kutumia anga hiyo ya kiroho na kimaanawi kuimarisha udugu na mshikamano wa Kiislamu.
Duru ya pili ya mashindano ya kimataifa ya Qurani ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kiislamu imepangwa kufanyika tarehe 10 Novemba ikiwashirikisha wanachuo kutoka nchi 38 za Kiislamu na zisizo za Kiislamu. 312133