IQNA

Makosa katika Quran iliyochapishwa na Wizara ya Wakfu Qatar

11:39 - November 09, 2008
Habari ID: 1706101
Nuskha moja ya Quran tukufu iliyochapishwa na kusambazwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar imeshudhiwa ikiwa na makosa kadhaa ya chapa.
Kwa mujibu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Masuala ya Kimataifa ya Taasisi ya Wakfu na Amali ya Iran, aya ya 44 hadi 111 za sura Nur zimefutika katika nuskha hii ya Quran tukufu na kuna makosa ya chapa katika suratul Furqan.
Aidha kurasa kadhaa za nuskha hiyo ya Quran zimepangika vibaya. Sura fupi za Juzuu ya 30 pia zinashuhudiwa baada ya Juzzu ya 18.
Nuskha hii ya Quran imetayarishwa na kamati ya usimamizi ya Wizara ya Wakfu ya Qatar na katika ukurasa wake wa kwanza kuna muhuri wa idhini wa kamati hiyo. Idhini ya chapa nambari 551/2006 pia inashuhudiwa katika ukurasa huo.
Gazeti lenye wasomaji wengi la As-Sharq limechapisha ripoti inayowakosoa vikali maafisa wa Wizara ya Wakfu ya Qatar na kutaka suala hilo lichunguzwe. Aidha gazeti hilo limetaka nakala zote za Quran zenye makosa zikusanywe. 317182
captcha