Msikiti na Chuo cha Sayansi ya Qur’ani cha al Saleh vilifunguliwa jana katika mji mkuu wa Yemen Sanaa. Sherehe za ufunguzi wa msikiti na chuo hicho zimehudhuriwa na Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye pia ni Mkuu wa Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu Mahdi Mustafawi na shakhsia wengine kadhaa wa ulimwengu wa Kiislamu.