Tovuti ya masuala ya kiitikadi, kisiasa na kiutamaduni ambayo huakisi shughuli za Idara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran inayoshughulikia masuala ya vyuo vikuu nchini imetunga leksikografia (usanidi kamusi au mu'jam) ya Qur'ani kupitia mtandao.
Akizungumzia suala hilo, Rafii', mkuu wa tovuti hiyo amesema kuwa, utafutaji wa masuala mbalimbali na hasa maneno na aya za Qur'ani Tukufu katika usanidi kamusi hiyo unatimia kwa msingi wa maneno ya Qur'ani. Amesema, kwa mfano mtu anapotafuta neno fulani katika leksikografia hiyo, humletea maneno kadhaa yanayoshabihiana na neno analotafuta kwa msingi wa minyambuliko tofauti ya neno hilo na kila anapobonjeza juu ya kila neno, humletea aya ambazo zimeyataja maneno hayo.
Amesema leksikografia hiyo ni msaada mkubwa kwa watafiti wanaotafuta maneno na vyanzo vyake vya kimsingi katika Qur'ani.
SAheikh amesema, umuhimu wa leksikografia ni kwamba, mtu anapokutana na neno au aya asiyojua inapatikana katika sura ua aya gani, anaweza kutumia leksikografia hiyo kupata aya au sura ambazo zina neno hilo. 395462