IQNA

Muhula wa kujiandikisha kwa ajili ya mashindano ya Qur'ani ya Kuwait wamalizika

12:33 - April 29, 2009
Habari ID: 1771599
Sekretarieti ya Wizara ya Waqfu ya Kuwait imengaza kuwa muhula wa kujiandikisha kwa ajili ya mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani yatakayofanyika chini ya anwani ya "Hii Ndiyo Nguzo Yangu", unakaribia kumalizika.
Habari hiyo imetangazwa na Naibu Katibu Mkuu wa Mfuko wa Waqfu wa wizara hiyo Muhammad Abdullah ambaye ameongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa lengo la kuimarisha thamani za Kiislamu zilizobainishwa katika kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Muhammad Abdullah amewataka watu wanaotaka kushiriki kwenye mashindano hayo ya Qur'ani kusajili majina yao haraka kabla ya muhula ulioainishwa haujamalizika. Amesema kuwa muda wa kujiandikisha kwa ajili ya mashindano hayo utamalizika tarehe 30 mwezi huu wa Aprili.
Afisa huyo wa Wizara ya Waqfu ya Kuwait amesisitiza kuwa malengo mengine ya mashindano hayo ni kuwahamasisha vijana wa rika mbalimbali kuhifadhi, kusoma tajwid na kutabadabari ndani ya Qur'ani Tukufu. 396036

captcha