IQNA

Watoto wafunzwe Qur'ani kwa kutumia njia wanazozipendelea wao

0:39 - May 01, 2009
Habari ID: 1772098
Watoto wadogo wanapaswa kufunzwa Qur'ani Tukufu kwa kutilia maanani mambo yanayowavutia kama michoro, visa na kadhalika.
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Hamid Idi, mhadhiri wa vyuo vikuu nchini Iran. Hamid Idi amesema kuwa watoto wadogo nawanapswa kufunzwa Qur'ani katika kipindi cha utotoni na kuongeza kuwa wazazi wanaotaka watoto wao waanisike na kuvutiwa na Qur'ani wanapaswa wao wenyewe wawe ni wasomaji wa kitabu hicho kitukufu ili watoto wao waathirike na suala hilo.
Amesema kuwa iwapo mtoto hatakuwa na malezi ya Qur'ani, itakuwa vigumu kutarajia kwamba atakuwa miongoni mwa wasomaji wa kitabu hicho.
Hamid Idi ameashiria hadithi nyingi zinazohimiza kuwafundisha watoto Qur'ani na akasema: Kuna mbinu tofauti za kuwafunza watoto Qur'ani ikiwa ni pamoja na kutumia visa, mashairi, uchoraji na kadhalika ambazo zinapaswa kutumiwa kwa mujibu wa hamu na chaguo la mtoto anayefunzwa Qur'ani. Amesisitiza kuwa kwa kutilia maanani kwamba aghlabu ya watoto wadogo huvutiwa na visa, maana ya aya za Qur'ani zinaweza kufundishwa kwa watoto kwa kutumia sanaa hiyo.
Vilevile amesisitiza juu ya kuwafunza watoto maana ya aya za Qur'ani kwa kutumia vitabu na CD za katuni za visa mbalimbali vyenye mafunzo na malezi ya Kiislamu. 396518
captcha