Mkurugenzi wa Darul Qur'ani Nasruddin Madukh amesema kuwa lengo la mpango huo ni kulea kizazi cha Qur'ani na kueneza utamaduni wa kuhifadhi kitabu hicho kitukufu katika familia za Kipalestina.
Msimamizi wa mpango wa al Shafii' Nadir Abdunnabi amesema kuwa moja ya malengo muhimu ya mpango huo ni kuwahamasisha wanafunzi kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kwamba sambamba na hayo kunatolewa mafunzo ya malezi, uendesha wa masuala ya idara, elimu ya komputa na lugha.
Mpango wa al Shafii' ambao ni makhsusi kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 8 hadi 12 unasimamiwa na taasisi ya kimataifa ya al Rahma. 397940