Bibi Rifqa Ahmad anasema kwamba hakudhani kuwa anaweza kuhifadhi Qur'ani nzima katika umri kama wake lakini amefanikiwa kufanya kazi hiyo kwa irada na uwezo wake Mwenyezi Mungu.
Amesema: "Nilianza kuhifadhi Qur'ani miaka mine iliyopita wakati wa kuasisiwa msikiti wa Darul Qur'ani jinari na nyumbani kwangu na nikaanza kushiriki kwenye vikao vya tajwidi." Anaendelea kusimulia kwamba alishindwa kuendelea kushiriki kwenye masomo ya Qur'ani msikiti hapo kutokana na udhaifu wa kuona na hapo ndipo alipochukua uamuzi wa kuhifadhi Qur'ani ili athibitishe kwamba anaweza kuhifadhi kitabu hicho licha ya tatizo la macho. 648444