IQNA

Saudi Arabia yazuia walio chini ya umri wa miaka 15 kushiriki Hija

14:02 - May 08, 2026
Habari ID: 3482215
IQNA-Licha ya kwamba safari za waumini kuelekea Hija zilianza wiki tatu zilizopita, serikali ya Saudi Arabia imepiga marufuku ghafla walio chini ya umri wa miaka 15 kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu.

Wizara ya Hija ya Saudi Arabia imetangaza kuwa kuanzia  haitaruhusu kila mwenye umri chini ya miaka 15 kuteleza ibada ya Hija mwaka huu. Taarifa hii imekuja wakati waumini kutoka nchi mbalimbali tayari wameingia katika ardhi tukufu kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hijja ya Tamatu’.

Katika miaka iliyopita, mamlaka za Saudi Arabia zilikuwa zimepiga marufuku kuingia kwa mahujaji walio chini ya miaka 12, lakini katika kutolewa kwa viza walikuwa bado wanawapa watoto ruhusa ya kusafiri. Jambo hilo linasemekana kuwa lilichangia ongezeko la vifo, hasa kutokana na joto kali lisilovumilika katika siku za Hijja.

Kwa msingi huo, Saudi Arabia imetoa uamuzi wa ghafla wa kuongeza kiwango hicho cha umri kwa miaka mitatu zaidi, na hivyo kuzuia kuingia kwa walio chini ya miaka 15. Wamesisitiza kuwa viza zilizokwisha kutolewa kwa watoto hao hazitakuwa na uhalali kuanzia tarehe 5 Mei, na watakaowasili nchini humo watazuiwa kuingia.

Uamuzi huo mpya unahusu raia wa mataifa ya nje pekee, wakati raia wa Saudi Arabia hawataathiriwa.

Salman bin Saleh, mwanaharakati wa utamaduni wa Saudi Arabia, amesema kwamba wananchi wa nchi hiyo wamezoea hali ya hewa na mazingira ya Saudia.

Kwa upande mwingine, Qadir Taha, mkurugenzi wa masuala ya Hijja wa Pakistan, amesema: “Ikiwa ni sheria, iwe kwa wote sawa.”

Wataalamu wa masuala ya Hija wanaeleza kuwa Saudi Arabia ilipaswa kutangaza vikwazo hivi kabla ya  kuanza safari za Hija mwaka huu na si katikati ya msimu. Wamependekeza kuwa Sheria iwe sawa kwa wote, na kama si hivyo, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) iingilie kati ili kuondoa ubaguzi huu wa wazi.

4350532

Kishikizo: hija saudi arabia
captcha