Washindani 71 wameshiriki katika mashindano hayo ambayo yamewashirikisha wanaume na wanawake katika vitengo tofauti vya kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi juzuu 15, 10 na 5 za kitabu hicho kitakatifu.
Marefa mashuhuri wa Qur'ani wamesimamia mashindano hayo ambayo yamehudhuriwa na wanazuoni na watu wengine wengi wapenzi wa Qur'ani.
Akizungumza katika mashindano hayo, mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu amesema kuwa mafunzo na kueneza mafundisho ya Qur'ani kote ulimwenguni ni sehemu muhimu ya shughuli za jumuiya hiyo, na amewashukuru viongozi wa Burkina Faso kwa kushirikiana katika kuandaa mashindano hayo.
Washindi wa mashindano hayo wametuzwa na kuzawadiwa zawadi nono kutokana na juhudi walizofanya katika mashindano hayo. 671216