Kituo cha upashaji habari cha Islamic Art Magazine kimeripoti kuwa nakala mbili zinazofanana na nakana hii ya Qur’ani ziliuzwa mwaka 2006 kwa bei ya dola milioni 10 na mwaka 2007 nakala kwa bei ya dola milioni 4.3.
Nakala hii ya Qur’ani yenye umri wa miaka 300 imetolewa katika majmui ya Abu Ja’far Sirajuddin Muhammad Bahador Shah Zafar (1775-1862) mfalme wa mwisho wa utawala wa Gurkani wa India.
Baadhi ya sehemu za Qur’ani hiyo nadra zimepambwa kwa maji ya dhahabu.
Nakala hiyo ya Qur’ani ya kale ina upana wa sentimita 14.5 na urefu wa sentimita 24. 670963