IQNA

Masomo ya tajwidi na fani ya daraja za Qur'ani kufanyika Qatif

15:18 - October 11, 2010
Habari ID: 2010792
Kituo cha taaluma ya Qur'ani katika mji wa Um al Hammam mkoani al Qatif kimeandaa masomo ya kutadabari Qur'ani Tukufu, elimu ya tajwidi na daraja za Qur'ani.
Kituo cha habari cha Qasid kimetangaza kuwa masomo hayo yatakashirikisha watu wa rika mbalimbali na wanaotaka kushiriki wamepewa fursa ya kujiandikisha hadi mwishoni mwa wiki hii.
Taarifa ya kituo hicho imesema kuwa masomo hayo yatajumuisha elimu ya juu ya tajwidi, fani ya daraja za Qur'ani Tukufu na sayansi ya Qur'ani.
Kituo cha Taaluma ya Qur'ani cha Um Hammam pia kitakuwa na masomo ya Qur'ani kwa ajili ya watoto wadogo. Kituo hicho ni miongoni mwa vituo muhimu vya taaluma ya Qur'ani katika eneo lenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia huko mashariki mwa Saudi Arabia. 672792
captcha