Mwakilishi wa IQNA barani Afrika ameripoti kuwa Wizara ya Majumba ya Makumbusho na vituo vya kukarabati nakala za Qur'ani huko Imarati hadi sasa imekwisharekebisha nakala zaidi ya elfu moja zilizochakaa za Qur'ani na kuzitoa zawadi kwa nchi za Kiafrika.
Mpango wa kukarabati nakala zilizochakaa za Qur'ani Tukufu kwa shabaha ya kuzilinda na kueneza hati za maandishi ya Kiarabu ulianza tarehe 2 Aprili na utaendelea hadi Jumatatu ya wiki hii.
Kwa mujibu wa mpango huo, raia wote wametakiwa kushiriki katika mpango huo kwa kukusanya vitabu na nakala za zamani za Qur'ani ambazo hawazitumii tena ili vitabu hivyo vifanyiwe ukarabati na kugawiwa kati ya watu wanaovihitaji kwa shabaha ya kuzidisha wasomaji Qur'ani. 995097