Kwa mujibu wa tovuti ya lexpressiondz masomo hayo ambayo yamedhaminiwa na Wizara ya Masuala ya Kidini ya Algeria yameanza kutolewa kwa wanafunzi wa shule za kidini za mji mkuu huo.
Sherehe za kuanza masomo hayo zimehudhuriwa na walimu pamoja na wakuu wa taasisi za kidini za mji huo. Lengo la kutolewa masomo hayo ni kutumiwa njia na mbinu mpya katika mafunzo ya masomo ya Qur'ani Tukufu katika shule za Qur'ani pamoja na kuwashawishi watoto wadogo kuhudhuria masomo ya Qur'ani katika shule hizo.
Wanaosimamia masomo hayo wanasema zaidi ya wanafunzi 300 wanasoma masomo ya Qur'ani katika shule za Qur'ani za mji mkuu wa Algeria na kwa hivyo masomo hayo yanapasa kutolewa kwa uangalifu na umakini mkubwa.
Masomo hayo maalumu yataendelea kwa muda wa wiki moja. 001312