IQNA

OIC yaitaka Sri Lanka iache kuchoma moto miili ya Waislamu

17:28 - February 24, 2021
Habari ID: 3473679
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito kwa Sri Lanka kuheshimu haki za Waislamu kuzikwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

Yousef Al Othaimeen, Katibu Mkuu wa OIC ameyasema hayo wakati akizungumza katika Kikao cha 46 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Amesema OIC inafuatilia hali ya Waislamu katika nchi zisizo za Kiislamu. Kwa msingi huo amesema OIC ina wasiwasi kuhusu Waislamu wa Sri Lanka kwani wananyimwa haki ya kuzikwa kwa mujibu wa mafundish ya Kiislamu wanapofariki kutokana na COVID-19. Amesema Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshatoa maelekezo ya namna ya kuzingatia sheria za Kiislamu za maziko wakati wa kuwazika Waislamu waliopoteza maisha kutokana na COVID-19.

Hivi karibuni Waislamu nchini Sri Lanka waliwasilisha malalamiko kwa Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kuhusu sera ya serikali yao ya kuchoma kwa lazima miili ya Waislamu wanaoshukiwa kupoteza maisha kutokana na corona au COVID 19.

Katika barua hayo hiyo, Waislamu wamesema utekezaji moto miili hiyo ya Waislamu si tu kuwa ni ukiukwaji wa haki zao za kidini bali jambo hilo pia linawaumiza sana hisia zao.

Katika malalamiko hayo ambayo yamewasilishwa kwa msaada wa Baraza la Waislamu Uingereza, familia kadhaa za Waislamu Sri Lanka zinasema mamia ya miili ya jamaa zao imechomwa moto pamoja na kuwa wataalamu wa afya katika ngazi ya kimataifa na kitaifa wamesema hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa corona husambazwa kupitia miili ya waliofariki.

Wakati huo huo, Waislamu wa Sri Lanka siku ya Jumanne waliandamana katika mji mkuu, Colombo wakitaka serikali isitieshe sera ya kuteketeza moto ya wenzao wanaopoteza maisha kutokana na COVID-19. Maandamano hayo yamefanyika katika siku ambayo Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan aliwasili nchini humo kwa ziara rasmi.

Waandamanaji hao walimhimiza Imran Khan, ambaye wiki mbili zilizopita aliwatetea, aihimize serikali ya Sri Lanka isitishe sera hiyo ya kuchoma moti miili ya Waislamu.

Inadokezwa kuwa tokea janga la corona lianze, maiti za Waislamu 200 waliofariki zimeteketezwa moto Sri Lanka kwa mujibu wa itikadi za Wabuddha na Wahindi ambao ndio wengi nchini humo.

Akizungumza mwezi Disemba, Hilmy Ahmed, naibu Rais wa Baraza la Waislamu nchini Sri Lanka, alisema kuchoma miili ya Waislamu ni ishara wazi ya ajenda ya "ubaguzi" , unaowalenga Waislamu waliyo wachache.

3474078

 

captcha