Katika barua hayo hiyo, Waislamu wamesema utekezaji moto miili hiyo ya Waislamu si tu kuwa ni ukiukwaji wa haki zao za kidini bali jambo hilo pia linawaumiza sana hisia zao.
Katika malalamiko hayo ambayo yamewasilishwa kwa msaada wa Baraza la Waislamu Uingereza, familia kadhaa za Waislamu Sri Lanka zinasema mamia ya miili ya jamaa zao imechomwa moto pamoja na kuwa wataalamu wa afya katika ngazi ya kimataifa na kitaifa wamesema hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa corona husambazwa kupitia miili ya waliofariki.
Mwezi Aprili mwaka jana na mwezi Januari mwaka huu, wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliiandikia barua serikali ya Sri Lanka wakiitaka iheshimu haki ya wanaozikwa.
Dr Lionel Bopage aliyeandika barua mwezi J iliyotumwa kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba serikali ya Sri Lanka inakiuka haki za Waislamu na Wakristo kwa kuchoma moto maiti za watu wanaofariki dunia kwa sababu ya ugonjwa wa Covid-19.
Inadokezwa kuwa tokea janga la corona lianze, maiti za Waislamu 200 waliofariki zimeteketezwa moto Sri Lanka kwa mujibu wa itikadi za Wabuddha na Wahindi ambao ndio wengi nchini humo.
Akizungumza mwezi Disemba, Hilmy Ahmed, naibu Rais wa Baraza la Waislamu nchini Sri Lanka, alisema kuchoma miili ya Waislamu ni ishara wazi ya najenda ya "ubaguzi" , unaowalenga Waislamu waliyo wachache.
"Serikali haijachukua hatua hiyo kwa misingi yoyote ya kisayansi," alisema. "Hawaonekani kufuata ushauri wa wataalamu wa magonjwa yanayotokana na virusi wala wanabaiolojia. Hii ni ajenda ya kibaguzi inayoendeshwa na baadhi ya watu waliyojumuishwa katika kamati ya wataalamu iliyobuniwa na serikali."