IQNA

TEHRAN (IQNA)- Katika mitandao ya kijamii kumesambaa kilpu ya Qarii Abdullah Khaled wa Pakistan akiwa anasoma aya za Surah Ibrahim.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Abdullah Khaled ni msoamo maarufu wa Qur'ani nchini Pakistan na katika klipu hii anasikika akisema aya za 31 na 34 za Surah Ibrahim katika Qurani Tukufu zisemazo:

31. Waambie waja wangu walio amini, washike Sala, na watoe katika tulivyo waruzuku, kwa siri na dhaahiri, kabla haijafika Siku isiyo kuwa na biashara wala urafiki.

32. Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito ikutumikieni.

33. Na akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na mchana kwa manufaa yenu.

34. Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.

 

4016564

Kishikizo: qarii ، qurani tukufu ، pakistan