IQNA

Mashindano ya Qur’ani yafanyika Pakistan katika Kumbukumbu ya Mashahidi wa Muqawama

21:05 - November 08, 2024
Habari ID: 3479718
IQNA - Mashindano ya usomaji wa Qur'ani Tukufu yalifanyika Rawalpindi, Pakistani kuwaenzi mashahidi wa muqawama.

Jumba la Utamaduni la Iran mjini humo liliandaa hafla hiyo kwa ushirikiano na Kituo cha Utamaduni cha Iran kilichopo Islamabad.
Zaidi ya maqari 40 walishindana katika sehemu mbili za wanaume na wanawake na vikundi viwili vya umri wa chini ya miaka 16 na 16 na zaidi, kulingana na Shirika la Iran Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu.
Jopo la waamuzi lilijumuisha idadi ya wataalam wa Qur'ani kama Qari Munawar Khan Ziaei na Hussein Chaqami.
Washindi hao walitunukiwa katika hafla iliyofanyika katika Jumba la Utamaduni.
Mkuu wa Jumba la Utamaduni la Iran Mehdi Taheri alihutubia katika hafla hiyo na kusisitiza kuwa, muqawama wa Kiislamu (mapambano ya Kiislamu) unatokana na mafundisho mazito ya Qur'ani Tukufu ambayo yanawafundisha wanadamu kutosalimu amri chini ya ukandamizaji na dhulma.
Vile vile amesisitiza haja ya kuimarishwa umoja baina ya Waislamu kwa kuzingatia maamrisho ya Qur'ani Tukufu ili kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa Kiislamu na kutetea ukweli na uadilifu.
Maonesho yaliyokuwa yakionyesha picha za Palestina na ukandamizaji wa Wapalestina unaofanywa na utawala wa Kizayuni pia yalifanyika kando ya mashindano hayo.

Quran Contest Held in Pakistan’s Rawalpindi in Memory of Resistance Martyrs

4246635

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: pakistan qurani tukufu
captcha