IQNA

Qurani Tukufu

Afisa wa Pakistan: Kueneza Maarifa ya Qur'ani ni wajibu wa kila Muislamu

20:13 - March 05, 2024
Habari ID: 3478454
IQNA - Waziri anayemaliza muda wake wa masuala ya kidini wa Pakistan amesisitiza wajibu wa kila Muislamu mwanamume na mwanamke kueneza elimu ya Qur'ani Tukufu.

Aneeq Ahmed alisema hayo alipokuwa akihutubia kwenye semina kuhusu ‘Maisha Yenye Lengo’ iliyoandaliwa na Asr School System huko Islamabad.

"Qur'ani Tukufu inatufundisha kuhusu kuchunguza ulimwengu na kanuni kamili za maisha na lazima tuifanye dunia hii kuwa mahali pa kuishi pa thamani," waziri huyo anayeondoka alisema.

Akizungumzia umuhimu wa kueneza ujumbe wa dini ya Kiislamu na maarifa, waziri huyo alisema kwamba wale wenye elimu na wale wasiojua kamwe hawawezi kuwa sawa.

“Qur’ani Tukufu itaendelea kuongoza akili ya mwanadamu hadi mwisho wa dunia na bila ya kuifahamu Qur'ani Tukufu, haiwezekani kumwelewa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na kumwelewa Mtume (SAW) ni muhimu katika kuifahamu Quran,” alisisitiza.

Alibainisha kwamba Allama Iqbal, msomi maarufu wa Pakistan, alisema kwamba kila Muislamu anapaswa kugeuza kila elimu ya ulimwengu kuwa Uislamu.

Aidha, alisema kuanza Utume wa  Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kulikuwa  ni mwisho wa zama za kale na mwanzo wa zama za kisasa.

3487430

Kishikizo: qurani tukufu pakistan
captcha