IQNA

Mazungumzo baina ya dini

Mtaalamu: Qur'ani Tukufu inamgeuza Maryam kuwa daraja kati ya Uislamu na Ukristo

20:18 - September 07, 2024
Habari ID: 3479397
IQNA – Maelezo ya Qu'rani Tukufu kuhusu Bibi Maryam (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-SA-) yanatumika kama "daraja" la kuleta Uislamu na Ukristo karibu zaidi, anasema msomi mwandamizi wa Kiislamu.

"Bibi Maryam (SA) ana jukumu muhimu katika historia ya dini za Mwenyezi Mungu; hakuwa tu mama wa nabii mkubwa bali pia umakini wa Qur'an juu yake umemfanya kuwa daraja kati ya Uislamu na Ukristo," amesema Ayatullah Ahmad Moballeghi alipokuwa akihutubia mkutano wa mazungumzo ya kidini katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini siku ya Alhamisi.

“Tabia au shakhsia yake inachangia katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya Waislamu na Wakristo,” aliongeza.

Katika hotuba yake, Ayatullah Moballeghi alifafanua kuhusu tabia ya Bibi Maryam (SA) kwa msingi wa Qur'an'.

“Bibi Maryam (SA) ni kama daraja la usafi na imani kati ya Uislamu na Ukristo na anachukuliwa kama alama ya utakasifu na uadilifu duniani,” alisema, akiongeza, “Hadhrat Maryam (SA) anatambuliwa kama mfano wa uchaji Mungu na maadili mema kati ya wanawake wote duniani, na maisha yake yamejaa ishara za Kimungu na miujiza ambayo yamemfanya kuwa daraja la kuleta Uislamu na Ukristo pamoja.”

Bibi  Maryam (SA) ana "nafasi ya juu" katika Uislamu na Ukristo, alisisitiza msomi huyo, akitaja kuwa jina lake limetajwa mara 34 katika Qur'ani Tukufu, na Surah nzima imetengwa kwa ajili yake, ikionyesha fadhila zake adhimu.

“Maisha ya Bibi Maryam (SA) yana miujiza na ishara za kimungu, kama kupata mimba kimuujiza bila kuingiliwa na kibinadamu, riziki ya kimungu, na kuzungumza kwa Nabii Isa (AS) akiwa mtoto mchanga, akithibitisha unabii wake na Tauhidi au itikadi ya Mungu Mmoja,” alisema.

Mtazamo wa pamoja kuhusu Bibi Maryam na Bibi  Fatimah (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao) unafungua njia mpya ya umoja kati ya dini, aliongeza.

Kongamano hilo liliratibiwa kwa ushirikiano na Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO).

4235258

Kishikizo: maryam
captcha